Kilimo na Ufugaji sehemu ya pili/ Biashara ya Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Awali ya yote ningependa kuomba radhi kwa kushindwa kuwakilisha makala hii kwa muda uliopangwa kutokana na kuharibika kwa kifaa changu cha kazi. Ninashukuru kupata nafasi ya kushirikiana nanyi tena mambo machache katika makala hii. Ufugaji ni sekta yenye faida nyingi kwa watanzania. Baadhi ya watanzania wamejihusisha katika ufugaji na kupata mafanikio makubwa. Sekta hii inaweza ikatumika katika kukuza mtaji, au katika kuleta mtiririko wa fedha. Kuna aina nyingi za ufugaji kutegemea na mtaji wa mfugaji na aina ya wanyama anaofuga. Kuna aina nyingi za wanyama na ndege wanaofugwa kwa ajili ya biashara, baadhi yao ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, kanga, batamzinga, kanga, kware, njiwa, sungura, nk. Ambao hutumika kwaajili ya matumizi ya nyama, au bidhaa za wanyama hao mfano maziwa na mayai. Katika makala hii tutajikita katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa ajili ya biashara, ungana nami ninapokuletea muendelezo wa makala iliyopita ikiwa ni mtiririko wa makala za biashara ya kilimo