Masomo kadhaa kutoka kwenye maisha ya Aliko Dangote




Kwa ajili ya kila mtu anayetazamia kuongezeka mahali alipo
Alhaji Aliko Dangote tunamuona na kumsikia tu kwenye mitandao na televisheni, wakati mwingine tumemfahamu kwa kutumia bidhaa yake inayouzwa hapa Tanzania. Ni mfanya biashara aliyefanikiwa zaidi Afrika na biashara zake zimeenea katika nchi nyingi.
Kufikia Januari 2015, Dangote alikadiriwa kuwa na thamani ya dola Bilioni 18.6 kufikia 2014. amejenga utajiri wake kupitia saruji, sukari na unga. Mwezi wa 4 2014, miezi michache tu kabla bei ya mafuta haijaporomoka, alitangaza kutoa dola bilioni 9 kwa ushirikiano na wakopeshaji wa ndani mwa Naijeria na wa nje ili kujenga kituo cha kusafishia mafuta cha binafsi na kiwanda cha mbolea na kiwanda cha kemikali nchini Naijeria. Mwezi wa 8 2014 akasema angewekeza dola bilioni 1 katika kilimo cha kisasa cha mpunga na viwanda vya kisasa vya kuzalisha mchele. Saruji yake ya Dangote yenye jina kubwa pia ilikuwa ikikamata masoko mapya Afrika, akiwa ametoa dola milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya Kenya na Niger. Mwezi wa pili 2014 Thamani yake ilikuwa dola bilioni 25 hivyo ilishuka kwa sababu ya udhaifu wa sarafu ya Naijeria na kushuka kwa mahitaji ya saruji. Pamoja na yote alitengeneza utajiri wake kwa kuwa mchuuzi baada ya kupewa mkopo na mjomba yake aliyekuwa tajiri.
mpaka hapo nadhani kuna mambo umejifunza lakini ninataka nikupitishe kwenye mambo 10
aliyopitia Aliko ili nawewe uweze kujifunza jambo.
1. Aliwahi kuajiriwa na mtu
Aliko aliwahi kumfanyia kazi ndugu wa baba yake aliyeitwa Sani Dangote. Alimtumikia Bwana wake kwa bidii aliishi msemo wake maarufu unaosema “kama ni lazima uongoze, ni lazima utumike.” Ni kipindi hiki Aliko alipata uzoefu mwingi, stadi mbali mbali na ujasiri.
Kwanza kabisa huwezi kufika popote usipokuwa na mwongozo wa kukuongoza, Mmiliki wa alibaba, Jack Ma aliwahi kusema “unapokuwa na umri wa miaka 20 hadi 29 kinacholeta maana ni kwamba upo chini ya bosi yupi, sio upo kwenye kampuni ipi….” Hivyo msingi wa kujenga biashara yako kufikia kwa Aliko, au kupanda ngazi na kuwa Meneja Mkuu wa Kampuni Fulani siku moja ni kuwa na mtu atakayekuongoza katika njia unayotaka kupita.
2. Alichukua mkopo ili kuanzisha biashara yake
Aliko Dangote alianzisha biashara yake kwa mkopo wa naira 500,000 (ambayo ni zaidi ya 35,000,000 kwa sasa) kutoka kwa mjomba wake au mwalimu wake. Alimfuata mjomba wake mwaka 1977 na kumwambia kuhusu mpango wake wa kuanzisha biashara na mjomba wake akampatia mkopo wa kuanzisha biashara hiyo. Hata hivyo, alipewa muda wa kikomo wa miezi mitatu na alilipa deni la mkopo wake ndani ya miezi mitatu.
(endelea kutembelea blogu hii na nitakwambia jinsi ya kupata mtaji)
3. Alikuza biashara yake kwa kuchuuza bidhaa
Sukari, mchele, tambi, chumvi, pamba, ulezi, kokoa, nguo na mafuta ya kupikia zilikuwa ni bidhaa alizoanza nazo kufanya biashara. Alikuwa akiingiza nchini Naijeria bidhaa hizi kutoka nchi zingie.
4. Aliunda mtandao imara wa biashara
Kwa vile uzalishaji haukukamilika hadi bidhaa zimfikie mtumiaji, Dangote alianzisha mkondo imara wa usambazaji ambao ulifanya bidhaa zake zisambazwe kwa haraka kuliko washindani wake. Katika kila Nyanja ya maisha, biashara, kazi, ujasiriamali, dini, nk. Ni lazima uje na kitu cha tofauti, washindani hawatakosekana lakini una nini cha kuwazidi?
5. Akaruka kutoka usambazaji hadi uzalishaji
Watu wengi hawajafahamu kwamba unaweza ukaanzia katika usambazaji kuelekea kwenye uzalishaji, wengi huamini kuzalisha kabla ya kuingia kwenye usambazaji mkubwa ni bora lakini Dangote baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi ya kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na kujenga mtandao, alibadilika na kuwa mzalishaji wa bidhaa alizokuwa akiingiza nchini. Katika moja ya maneno yake alifunua kwamba kubadilika kutoka katika kuingiza bidhaa nchini na kuwa msambazaji kumekuwa ndio hatua bora zaidi aliyowahi kutembea. Badiliko hili likaanzisha Dangote Group, Muunganiko wa makampuni unaongoza makampuni zaidi ya 13.
6. Akatengeneza Chapa (Brand)
Dangote alijenga chapa kubwa kwa  ajili ya biashara zake. Anathibitisha haya katika mahojiano Fulani kwa kusema, “Kufanikiwa katika biashara ni lazima uunde chapa na kamwe usiiharibu. Moja ya jambo lililonisaidia dhidi ya washindani wangu nilipoingia kwenye uzalishaji ilikuwa ni chapa yangu (Dangote), ambayo niliijenga katika safari yangu ya kibiashara.”
7. Akauza vitu vyenye thamani ya chini
Ili kutimiza utume wake wa kupata wateja waaminifu, Dangote alifuata kanuni maarufu ya kuwashinda washindani, alianza kuuza bidhaa zake za kiushindani kwa bei nafuu kulingana na bei za washindani wake.
8. Akapata mafanikio makubwa
Stadi na uwezo aliokuwa nao Dangote wa kutengeneza mtandao na uwezo wake wa biashara ulimpatia mafanikio ya kuvunja rekodi aliyohitaji ili biashara yake kufanikiwa. Mafanikio yake makubwa zaidi yaliibuka pale alipopata leseni ya kuingiza nchini saruji.
9. Anafanya kazi kwa bidii
Kama mfanyabiashara mwenye hekima, Alhaji Aliko Dangote anatumia muda wake mwingi kutengeneza mipango na kuwazua jinsi ya kukuza biashara yake. Ripoti zinasema kwamba huwa analala saa nane alfajiri na kuamka saa kumi na moja alfajiri kila siku. Unaweza hiyo?!
10. Anashika sheria za nchi
Tofauti na wafanya biashara wengine wajanja wajanja, Dangote ni mtu mwenye heshima ya uaminifu na hapendi kona kona inapofikia suala la kuenda sawa na sheria na kanuni za uendeshaji wa biashara. Anatunza kumbukumbu ya madeni na wadaiwa wake pamoja na kumbukumbu zake za kulipa kodi katika hali nzuri na anapenda kusema “biashara inapaswa kufanyika kwa jinsi zinavyoongozwa na watunga kanuni” akimaanisha kwenye bishara ili ufanikiwe njia za mkato sio hekima, na ujanja ujanja huua biashara. Ndio maana amesimama hata leo.
Hayo ni baadhi ya mafunzo machache tunayoweza kujifunza katika safari ya bwana Aliko Dangote. Na ninakualika endelea kufuatilia tovuti hii kwa ajili ya visa vingine vya watu mashuhuri, watu wa hapa nchini, na hata wa mtaani kwako utawaona katika makala zinazofuata.






Comments

Popular Posts