Unajua kutengeneza pesa kwenye uchumi mpya?
Ni mambo ya watoto!
Siku Fulani iliyopita,
rafiki yetu mpendwa alitutembelea nyumbani kwetu Afrika ya Kusini. Kijana wake
wa miaka 14 alizaliwa karibu sawa na mtoto wetu mdogo wa kike, na walisoma
chekechea pamoja. Nitamwita “John” kwa ajili ya kisa hiki kidogo, ambacho kwa
namna nyingine ni kweli.
Mama yake alianza kwa
majivuno na kusema, “John ni mfanyabiashara hakika,” kiuhalisia mama wote
wanjivunia watoto wao, kwa nini yeye awe tofauti?
Basi, akaendelea
kusema, “Wakati mwingine anatengeneza hadi randi 5000 kwa kutengeneza kurasa za
mitandao ya kijamii na kuziuza.
“Anafanya nini?”
Nilishangaa.
“Ah, hiyo sio kitu. Anafanya
hivyo akihitaji fedha za ziada.”
“Sawa… nini kingine
anachofanya?”
“Hivi karibuni alifanya
mazungumzo kwa ajili ya kitu Fulani cha kuchezea kutoka India, ili kukisambaza
Afrika Kusini”
“Alifanya nini?!”
Akasema, “Huwa
anakwenda kwenye Internet na kufanya utafiti wa bidhaa na bei, na kutafuta
vyanzo vya bei nafuu kwa ajili ya vitu kama ubao wa kuchezea Kriketi, na vitu vingine
ambavyo watoto wanapenda.”
Nikauliza kwa upole ili
tu nijihakikishie, “Unazungumzia John na sio baba yake?”
“Wakati mwingine John
humuomba baba yake amuwakilishe, pale anapohitaji mtu mzima.”
“Enhee!. . . Kwa hiyo
anamuajiri baba yake mwenyewe!”
“Angalia, John sio
mtoto pekee anayefahamu jinsi ya kutengeneza pesa kutoka kwenye mtandao.”
Kufikia hapo, nikacheka
na kusema: “kufikia hapo upo sahihi! Joe Gebbia, Brian Chesky, Nathan
Blechaczyk (mmoja wa walio anzisha Airbnb): Evan Spiegel, Reggie Brown na Bobby
Murphy (Walioanzisha Snapchat) na pia, Mark Zuckerberg!”
“Hawa jamaa walikuwa
watoto tu kulinganisha na watu kama mimi. Na bado walikuwa wamekwisha kujenga
biashara ambazo ni kubwa kuliko pato la taifa la nchi nyingi za Kiafrika!”
Lakini hapa kuna jambo
la “kushangaza”
“John” ni mtoto wa
kiafrika. Kama vile Anesi, na kaka yake, Osine, kutokea Nigeria ambao
niliwazungumzia mwaka 2015. Watoto ambao walitengeneza kitafutaji (Browser)
Hata kabla hawajaingia umri wa balehe?
Hii inamaanisha kwamba
Zuckerberg anayefuata labda anaishi nyumbani kwako, akizunguka tayari akiwa
anacheza na Lego na labda akifikiria kuhusu maroboti au zaidi!
Nyumbani kwangu
mwenyewe, binti yetu mdogo huwa anafanya mambo yote “ya kiteknolojia” wakati
watu walipomaliza Tovuti ya Kwese, nilimwita na nikamuuliza, “hii ina iko
vizuri?”
Alienda kwenye kona
akasema, “iko poa sana, lakini ningeweza kubadilisha hiki na hiki.”
Nikamwambia, “ngoja
nitafute pa kuandika mwanangu.”
Akasema, “utanilipa!”
Nikamwambia, “sema
gharama yako.”
Nikauliza swali rahisi:
“unafahamu kweli jinsi ya kutengeneza fedha kwenye uchumi huu mpya?”
Katika uchumi mpya,
itakuwa ni kuhusu uwezo wetu wa kuachilia mitizamo ya zamani kuhusu mali, na
jinsi ya kutengeneza mali. Lazima si tuwawezeshe tu watoto wetu; lazima
tuwaamini katika siku zetu zote zijazo.
Mwisho wa juma hili,
fanya mahojiano kidogo na uchunguze kile ulichofanya na simu yako ya
smartphone:
Ni tovuti gani
ulizotembelea, na kwa nini?
v Je! Ilikuwa kwa ajili ya kutafuta kitu?
v Je! Ilikuwa kwa ajili ya kuuza au kununua kitu?
v Ili kuwa kwa ajili ya kuburudika?
v Je! Ilikuwa ni kwa ajili ya kuwasiliana na marafiki
na familia?
Kama kimsingi ilikuwa
ni kwaajili ya kuwasiliana na watu, au ubadilishe tabia yako, au itakubidi
umfanyie kazi “John” siku moja … (Lakini haitakuwa mbaya, maana angalau utakuwa
na kazi.)
Katika mambo yote
unayofanya kwenye mtandao, je ulitengeneza fedha yoyote, endeleza kazi yako au
piga teke ili kuanzisha ule mwanzo wa biashara yako?
Ninamfikiria John
mdogo. Ana miaka 14, na tayari ameshaelewa uchumi mpya. Wow!
Hebu na tuingie kazini!
Tuna bara zima la kufanyia marekebisho … Tena haraka!
Comments
Post a Comment