Vifaa Vyako vya Kazi

Jitayarishe kufanya mabadiliko katika kazi yako.
Siku zote wekeza katika “vifaa vyako vya kazi”
Muda mfupi baada ya mimi kumaliza shahada yangu ya uhandisi huko Uingereza, ilinibidi kufanya kazi katika kituo cha uzalishaji huko Uingereza ili kupata “uzoefu wa kivitendo” kama walivyoiita kazi hiyo. Mafundi wengi ambao walikuwa pale kwa miaka mingi, walikuwa na ratiba Fulani ambapo niliweza kupata baadhi ya “vitendo na uzoefu wa maisha halisi.”
Inashangaza mara zote kwamba ni kanuni za muhimu kiasi gani unaweza ukapata, ambazo hata ukienda kufanya kitu kingine tofauti kabisa katika maisha yako zitakufaa.
v  Jisikie kiburi juu ya vifaa vyako vya kazi.
Kila fundi alikuwa na “boksi la vifaa vya kazi” ambavyo walivitunzaa kwa upendo. Ilikuwa ni kama “ibada ya mwisho.” Ilipofika mwisho wa kila siku, walikuwa wakiringishiana vifaa vyalivyoweza kupata, na kile walichofanyia vifaa hivyo. Walisafisha vifaa vyao mara baada ya siku kuisha.
Kununua na kuwekeza katika vifaa vilivyo bora ili ichukuliwa kuwa wajibu binafsi wa fundi yoyote, na sio mwajiri.
“Ninalisha watoto wangu kwa vifaa hivi, au sio?” mmoja wao aliwahi kunieleza hili kwa kiingereza chake kibovu.
Turuke mbele:
Mara zote nilikuwa nikipoteza kalamu yangu ya plastiki. Kisha mtu mmoja akaniambia, “usingeipoteza kama ungewekeza kwenye kalamu sahihi.”
“Dah!” nikawaza. “hii ni kama vile mafundi wazungu wa zamani na vifaa vyao.”
Siku ile, niliondoka nikaenda kujinunulia seti nzuri ya kalamu. Na mara moja nikaacha kupoteza kalamu!
Swali: “Vifaa vyako vya kazi” ni vipi?
Je! Una komputa? Kila mtu anayeendesha biashara ya kisasa, au anafanya kazi katika utaalamu fulani, lazima awe na laptop.
Komputa sio hata “kifaa” ni “boksi la vifaa” ambalo ndani yake mnawekwa vifaa vyote vya kisasa.
Je! Upo kwenye mtandao? Je! Una mtandao kweenye biashara yako na nyumbani kwako?
*kama sio, ni bora uuze gari lako, kama unalo, na utembee, lakini lazima uwe na komputa na uwe kwenye mtandao wakati wote.
*kama una nyumba kubwa, ina hekima zaidi katika ulimwengu wa sasa kuwa na nyumba ndogo yenye mtandao, kuliko nyumba kubwa isiyo na mtandao.
*Ingeonekana kuwa na hekima zaidi kuwa na gari dogo, au kutokuwa nalo kabisa,na uwe na uwezo wa kumudu komputa na Mtandao kwa ajiliya biashara na familia yako, kuliko kuwa na gari kubwa au vyovyote vile.
*wale wanaoelewa kile ninachozungumza hapa wapo kwenye nafasi nzuri ya kufanya mabadiliko katika kazi zao kulingana na inavyohitajika kama matokeo ya mabadiliko ya ghafla kazini, na kwenye kazi tunayofanya.
Kazi yoyote unayofanya, au unayopanga kufanya siku za mbeleni, unapaswa kukuza “boksi lako la vifaa” kulingana na mabadiliko ya nyakati zijazo. Ninataka uwe umejiandaa. Kumbuka nilichowahi kusema kuhusu mtazamo wako? Na kuhusu kufikiria mwisho wa upeo wa mwisho wa upeo wa leo?
Kama nilivyokwisha wahi kusema, “mapinduzi ya mitandao ya simu” yamekwisha kusafisha njia kwa ajili ya “Mapinduzi ya kimtandao.” Kama mtandao ungekuwa ni bahari, basi kile unachokiona leo ni ufukwe tu. Mtandao utabadilisha hata vijiji vyetu. Siku zijazo, mashine ya kusaga mtaani kwako itatumia mtandao, hata kuweka oda na kutunza kumbukumbu ya rasilimali. Hata shule ya kijiji itabadilishwa kwa mtandao.
Utaona yakitokea. Sehemu Fulani, mtu Fulani tayari anahangaika kutafuta suluhisho. Ni miaka kumi tu iliyopita, kama ningepaswa kukwambia, “Wanavijiji katika sehemu za  ndani kabisa mwa Afrika na Tanzania wangekuwa tayari kupokea pesa kutoka sehemu yoyote ulimwenguni ndani ya dakika tano au hata pungufu, “ ungesema nini?
Ninyi ndio mmeitwa kufanya mambo kama haya kutokea. Ni wakati wenu.
Je Boksi lako la vifaa lipo tayari?


Comments

Popular Posts